Mwenyekiti wa Baraza la
Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hashim Juma Issa
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo mchana, kuhusu kongamano litakalo wakutanisha wazee wote bila
kujali itikadi za vyama vyao litakalo jadili mustakabali wa taifa
kuelekea uchaguzi mkuu litakalofanyika kesho ukumbi wa Hoteli ya Blue
Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeandaa kongamano la wazee
ambalo litafanyika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam kesho.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari leo mchana Mwenyekiti wa Baraza
la Wazee la chama hicho, Hashim Juma Issa alisema kongamano hilo
litawahusisha wazee wote nchini bila ya kujali itikadi za vyama vyao.
Alisema
dhima kubwa ya kuanzisha kongamano hilo ni kuwapa elimu wazee bila
kujali itikadi zao za kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu.
“Wazee
wengi wamekuwa hawafahamu nini majukumu yao kama wazee lakini kongamano
hili litakuwa ndiyo chanzo kikubwa cha kuwafahamisha wazee majukumu yao
hasa katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi,” alisema Issa.
Alisema
kila mtu anafahamu binadamu huwa anapitia hatua muhimu za maisha nazo
ni utoto,ujana na utu uzima hivyo hamna budi wazee hawa kuelewa lengo
kuu katika katika uchaguzi mkuu huo kuwa katika mstari ulinyooka.
“Kumekuwa
na tabia ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwatumia wazee kwa ujanja tena
hasa wakiwa na matatizo na kuwabagua wa vyama vingine lakini sisi katika
kongamano hili hatutobagua mzee wa chama chochote katika kongamano hili
kwani wazee wote ni hazina,”alisema
“Hakuna
asiyefahamu kuwa kwa sasa nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao
uchaguzi huu utakuwa ni mkubwa na wa aina yake hivyo kwa kuwaita wazee
hawa itakuwa ni muendelezo wa kupata hekima zao kama wazee”alisema.
Issa
alisema katika uchaguzi mku wazee wana jukumu kubwa la kuhakikisha
kushiriki kikamilfu katika zoezi zima la kujiandikisha na kupiga kura
ipasavyo.
Alisema
hatua hiyo haina budi kuwasahawisi watoto na watu wakubwa na wajukuu
kushiriki kwa ukamailifu katika tukio hili kwani kila mtu anahitaji
mabadiliko katika nchi.
Hata
hivyo Issa alisema wazee pia wana jukumu kubwa la kutatua migogoro
,kushawisi na kusimamia maadili lengo likiwa ni uthubutu wa kukemea
viongozi wanaopata madaraka kwa njia ya rushwa na ufisadi.
Alisema wanahitaji wazee watakaosimama kidete na kupaza sauti zao katika kukemea maovu na watenda maovu bila kuona haya.
Alisema
katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa chama
hicho Wilbroad Slaa huku mada mbalimbali zitatolewa na Mabere Marando
pamoja na viongozi wa dini ili kuwapa elimu wazee kutokana na maadili ya
nchi kumomonyoka kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment