utt

.

line

line

line of success

line of success

Tuesday, July 14, 2015

UKAWA vimetangaza rasmi Mgombea wao Soma hapa>>>

Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA vimetangaza rasmi kufikia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Akitangaza makubaliano hayo mara baada ya kumalizika kwa kikao kirefu kilichokuwa kikijadili mustakabali wa kumpata mgombea urais pamoja na ugawanaji wa majimbo mapya, mwenyekiti mweza wa UKAWA James Mbatia amesema kuwa umoja huo umemteua mgombea ambaye ni chaguo la watanzania.
Mbatia amegoma kutaja jina la mgombea aliyepitishwa na umoja huo kwa madai kuwa anaandaliwa utambulisho maalum utakaoambatana na shamra shamra.
Kuhusiana na mgombea wa CCM Dkt John Magufuli, viongozi hao wamesema kuwa hawatishiki naye, na wala hawamfikirii, na kusisitiza kuwa mgombea ambaye ni chaguo la watanzania atatoka UKAWA na atatangazwa siku chache zijazo.

No comments:

Post a Comment