utt

.

line

line

line of success

line of success

Tuesday, June 30, 2015

Maonyesho ya Saba Saba yatafunguliwa na Rais Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete  anatarajiwa kufunungua Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) hapo kesho Julai mosi. Maonyesho hayo yaliyoanza Juni 28, yatafikia kilele Julai 7 na yanatarajiwa kukuza sekta ya uwekezaji kutokana na ushiriki wa nchi nyingi. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Jacqueline Maleko amesema nchi 25, kampuni za nje 400 na ndani 1,700 zinatarajiwa kushiriki kwenye maonyesho haya. Ameongeza kuwa maonyesho hayo ni fursa nzuri kwa wananchi na wafanyabiashara kukutana na wenzao kutoka mataifa mengine. Katika hatua nyingine amesema kuwa Julai 3, itakuwa siku maalumu kwa wanafunzi kuanzia wa shule ya awali, msingi, sekondari na vyuo vikuu na wataingia kwa makundi na kupata punguzo la kiingilio badala ya kulipa Sh4,000 watalipa Sh1,000.Kikwete

No comments:

Post a Comment