Meneja
mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Ravinshankar
Venkatrama ( wa pili kushoto) akiwa na timu ya wafanyakazi wa kampuni
hiyo watakaokua wanatoa huduma katika Banda la MO ASSURANCE lilipo ndani
ya mabanda ya MeTL Group kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya
Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa,
jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa wa kampuni ya MO
ASSURANCE, Mariot Ndomba, Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO
(MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack pamoja na Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya MO ASSURANCE, Esther Moringi.
MO
Assurance kampuni ya bima inayohudumia nchi nzima kwa kutoa huduma
mbalimbali za bima za majanga ikiwemo ajali ya moto, bima ya wizi, bima
za ajali mbalimbali.
“MO
Assurance tunapatikana ndani ya jengo la CRDB gorofa ya nane, mtaa wa
Azikiwe ambapo tunatoa huduma mbalimbali za bima.” alibainisha meneja
masoko msaidizi, Esther Moringi.
Aidha,
kwa sasa MO Assurance yenye kauli mbiu ya ‘Amani zaidi, Uhakika zaidi’
ina matawi sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Singida, Arusha na
kwingineko. Pia kwa sasa ni miongoni mwa makampuni ya bima nchini
yaliyofanikiwa ikiwemo kutoa huduma kwa wateja wa aina tofauti wakiwemo
wa ndani na nje wanaoishi nchini.
Kampuni ya MO Assurance ni kampuni Mama ya MeTL Group ambapo unaweza kuwasiliana nao kupitia barua pepe: infomoa@moassurance.co.tz ama kutembelea mtandao wao kupitia : moassurance.co.tz
Kutoka
kushoto ni Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE),
Ravinshankar Venkatrama, Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya mo
ASSURANCE, Esther Moringi, Afisa wa MO ASSURANCE, Mariot Ndomba pamoja
na Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE),
Tawheeda Isaack katika picha ya pamoja wakiwa tayari kutoa huduma kwa
wateja mbalimbali watakaotembelea katika Banda la MeTL Group lililopo
kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam
yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya
Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack akipiga ‘selfie’ na wafanyakazi wenzake.
Ofisa
Mtendaji wa Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda
Isaack katika picha ya pamoja na mbunifu wa mavazi nchini, Ally
Rehmtulah alipotembelea banda la MO ASSURANCE.
Muonekano
wa nje wa banda la kampuni ya MO ASSURANCE ndani ya maonyesho ya 39 ya
biashara ya kimataifa yalioanza kurindima katika viwanja vya Sabasaba
katika barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment