Meneja
Masoko wa kampuni ya Brightermonday Tanzania, Lugendo Khalfan ndani ya
hema la banda la Jakaya Kikwete akiwa tayari kukuhudumia wewe mtanzania
utakayetembelea banda lao katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya
kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, yanayoendelea kurindima kwenye viwanja
vya Mwl. J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Watafuta
ajira kote nchini Tanzania wamehamasishwa kujisajili na tovuti ya
Brighter monday ili wapate fursa ya kuunganishwa na watoa ajira.
Akifanya
mahojiano na mtandao wa habari wa modewjiblog.com, Meneja Masoko wa
Brighter monday Tanzania Khalfan Lugendo, amesema usajili huo ambao ni
bure, utamwezesha mhusika kupata taarifa mbalimbali na kuweza kuomba
nafasi tofauti za kazi ambazo zimewekwa katika tovuti hiyo.
Amesema
Brightermonday inajivunia kuwa ndio tovuti namba moja ya ajira nchini
Tanzania kwa kuwa idadi ya kazi wanazoziweka katika mtandao huo ni
nyingi kuliko chanzo chochote kile cha ajira nchini Tanzania.
Bw.
Lugendo ameongeza kuwa kwa mwaka jana 2014 waliweza kuweka nafa za
ajira 30,000 na hivyo kuwarahisishia waajiri mchakato mzima wa kuajiri
na kupata watu wenye viwango bora zaidi.
Aidha
ametoa wito kwa watu wote wanaotembelea maonyesho ya mwaka huu ya
kimataifa ya biashara Sabasaba, kutembelea banda lao lililopo katika
hema la Jakaya Kikwete ambapo watapata maelekezo kuhusu namna ya kuweza
kupata ajira kwa urahisi.
Key
Account Manager wa Brightermonday Tanzania, Gloria Nyiti kwenye sehemu
maalum ya kupokea wageni katika banda lao lililopo ndani ya hema la
Jakaya Kikwete.
Wafanyakazi
wa Brightermonday Tanzania wakitoa huduma kwa mmoja wa wateja
aliyetembelea banda lao lilipo ndani ya hema la Jakaya Kikwete kwenye
maonyesho sabasaba.
Gloria Nyiti akiwahudumia watafuta ajira katika banda la Brightermonday lililopo ndani ya hema la Jakaya Kikwete.
Gloria
Nyiti akitoa maelekezo ya namna ya kujisajili kwenye mtandao wa
Brightermonday kwa mmoja wa wateja aliyetembelea banda lao kwenye
maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kupamba moto jijini Dar.
Timu
ya wafanyakazi wa Brightermonday Tanzania wakiwa nadhifu katika banda
lao tayari kuwahudumia wateja kwenye maonyesho ya Sabasaba.
No comments:
Post a Comment