utt

.

line

line

line of success

line of success

Monday, July 13, 2015

Lowassa Sasa Kuhamia Ukawa,Ni baada ya mbowe kumuomba sana, Dk Slaa amkataa vikali, Asema yupo tayari kurudisha kadi ya chama,Asababisha Mpasuko mkali cdm Soma Hapa>>>>>

Hali ndani ya chadema imezidi kuwa tete mpaka Sasa baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. SLAA kutishia kurudisha kadi ya CHADEMA na kuachana na siasa za Chama hicho kama MBOWE ataendelea kumshawishi na Kumuomba LOWASSA ajiunge na Chama hicho ili awe Mgombea wao wa Urais.
Dr. SLAA ameonyesha msimamo huo Muda mfupi kabla ya LOWASSA hajazungumza na Waandishi wa Habari Nyumbani kwake Masaki kuhusiana na Hatima yake hiyo .
Slaa amekihakikishia chanzo chetu cha Habari kwamba yeye humuungi mkono MBOWE kwenye mpango wake huo wa kumtaka LOWASSA.
kijana mmoja wa CHADEMA ambaye yupo karibu na MBOWE amethibitisha kwamba MWENYEKITI wao huyo yupo tayari hata kumfukuza Chama SLAA ili LOWASSA awe Mgombea wao. anasema MBOWE anaamini kwamba LOWASSA ataipeleka CHADEMA madarakani.
Kwa sababu ya mpasuko huo, timu ya mkakati ya LOWASSA imeamua kuahirisha mkutano wao na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo saa Tano asbh hii kama ambavyo Mbowe ameomba ili kwanza wamalize tofauti zilizojitokeza Kati yake na SLAA.
Ikumbukwe kwamba hivi Sasa SLAA ana mvutano mkubwa na viongozi wenzake wa UKAWA ambapo analazimisha yeye ndio awe Mgombea.
Tayari Mzee EDWIN MTEI ametumiwa ndege ili aje Dar haraka kumshawishi SLAA akubali kumpisha LOWASA kugombea urais.

No comments:

Post a Comment