Diwani
wa kata ya Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Slaa
akiwasili mkutanoni kwa ajili ya kuwahutubia wananchi katika uwanja wa
shule ya msingi kitunda mwishoni mwa wiki ambapo alieleza mafanikio
yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha uongozi na kukamilisha ahadi
mbalimbali alizokuwa amezitoa.
Baadhi
ya madiwani na viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya
pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa muda mfupi baadaya
kuhutubia mkuatano wa hadhara kuelezea mafanikio yake mwishoni mwa wiki.
Mmoja
wa wawakilishi wa kikundi cha vijana akipokea fedha kwa niaba ya
wenzake kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala ambazo alikuwa amewaahidi
wakati wa mkutano wa Meya huyo kuelezea mafanikio yake katika uongozi.
Mmoja
wa wawakilishi wa kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya
wenzake kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala ambazo alikuwa amewaahidi
wakati wa mkutano wa Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wakishangilia kwa furaha baada ya kuguswa na hotuba ya Meya Jerry Slaa.
Wasanii mbalimbali pia walikuwepo kwenye mkutano huo kwa ajili ya kutoa burudani.
-Atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Ukonga
Diwani
wa kata ya Gongo la Mboto,Jerry Slaa ameainisha mafanikio aliyotekeleza
katika kipindi cha miaka 5 tangia achaguliwe kuwa Diwani na Meya wa
Manispaa ya Ilala ambapo pia alitimiza ahadi mbalimbali alizokuwa ametoa
kwa wakazi wa kata za manispaa ya Ilala.
Slaa
alivipatia msaada wa fedha vikundi vya VICOBA alivyokuwa ameviahidi
kuvisaidia,Genereta za kutoa nishati za kuendeshea miradi kwa vikundi
kwenye maeneo yasio na umeme,vifaa ya michezo kwa vijana na hati za
uthibitisho wa ujenzi wa barabara zitakazojengwa kwa madiwani wa kata
za jimbo la Ukonga.
Slaa
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi alitangaza
mafanikio hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya
msingi ya Kitunda iliyopo jimbo la Ukonga jana ambapo pia alitangaza
nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama cha Mapinduzi
katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Baadhi
ya mafanikio aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake
aliyabainisha kuwa ni katika sekta ya elimu- ambapo mazingira katika
shule mbalimbali yameboreshwa,afya-ambapo vituo vipya vimejengwa na
vingine kupatiwa vifaa na dawa,miradi ya maji na ujezi wa barabara
kwenye kata ya Gongo la Mboto na kata zote za Manispaa ya Ilala.
“Kutokana
na mafanikio yaliyopatikana nawaomba wananchi wa jimbo la Ukonga
mniunge mkono kwa kinichagua niwe Mbunge wenu katika uchaguzi mkuu ujao
ili nizidi kuwatumikia na kushirikiana nanyi kuleta maendeleo katika
jimbo hili la Ukonga ambalo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali
za maendeleo”Alisema.
Alisema
wakazi za jimbo la Ukonga wanahitaji Mbunge ambaye atakuwa bega kwa
bega na wananchi katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi. “Bado
tunahitaji kuboresha zaidi huduma za kijamii kama vile shule,
hospitali ,maji safi,kubuni miradi ya maendeleo ya akina mama na vijana
kwa kuwa naelewa matatizo ya jimbo hili na baadhi yake nilishaanza
kuyavalia njuga nikiwa diwani, mkinichagua kuwa mbunge wenu nitaendeleza
safari ya kuleta maendeleo.”
Mkutano
huo wa Meya Jerry Slaa ulihudhuriwa na mamia ya wakazi wengi wa jimbo
la Ukonga ambao wengi wao walipokea tamko hilo la kutangaza nia kwa
furaha na baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa kiongozi huyo anaelewa
matatizo ya wananchi wa Ukonga na ni mtu wa watu ambaye amekuwa
akitekeleza majukumu yake ya kazi kwa kujali watu wa aina zote.
No comments:
Post a Comment