Majengo
ya zahanati yanayoendelea kujengwa na mara yatakapokamilika yanatarajia
kugharimu jumla ya shilingi 88,703,000/= na litawahudumia wakazi 5,190
wanaoishi katika kaya 865.
WANANCHI
wa Kijiji cha Ibaga,tarafa ya Kirumi,wilaya ya Mkalama,Mkoani Singida
wanatarajia kutumia jumla ya shilingi 88,703,000/= kwa ajili ya
kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho iliyoanza kujengwa mwaka
2013.
Hayo
yamesemwa na afisa mtendaji wa Kijiji cha Ibaga,Bwana Hassani Kiyungi
wakati akitoa ufafanuzi juu ya gharama zinazotarajiwa kutumika
kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo inayosubiriwa na wakazi 5,190
wanaoishi katika kaya 865.
Aidha
afisa mtendaji huyo amefafanua kwamba mpaka sasa mradi wa ujenzi wa
zahanati hiyo umegharimu jumla ya shilingi 24,704,000/=,ambazo kati ya
kiasi hicho cha fedha,nguvukazi ya wananchi zimeokoa shilingi
15,650,000/=,serikali kuu shilingi (CBD) 5,000,000/= na michango ya
wananchi ni 4,054,000/=.
Kwa
mujibu wa mtendaji huyo ili waweze kukamilisha ujenzi wa mradi huo
mpaka sasa bado zinahitajika jumla ya shilingi 63,999,000/= na kwamba
kwa maana hiyo kulingana na hali ya hewa iliyowakumba wananchi,alitumia
fursa hiyo kuiomba serikali kuu iwasaidie kukamilisha mradi huo ili
kunusuru afya za wananchi wa Kijiji cha Ibaga.
Hata
hivyo mlinzi huyo wa amani wa Kijiji ameweka bayana kwamba zahanati
hiyo itakapokamilika itawasaidia wananchi kupata huduma za afya ya
matibabu kwa karibu,kwani mpaka sasa wananchi hufuata huduma katika
Kituo cha afya kilichopo Kijiji cha Mkalama na wengine Kijiji cha Ilongo
umbali wa kilomita tano kutoka hapo.
Aidha
afisa mtendaji huyo hata hivyo amebainisha pia kwamba wananchi wengine
wa Kijiji hicho hufuata huduma za afya katika Hospitali ya Misheni
Haydomu,wilayani Mbulu,Mkoani Manyara,Hospitali ya misheni
Nkungi,wilayani Mkalama na wengine wilayani Iramba.
Amefafanua
kuwa mara zahanati hiyo itakapokamilika itawasaidia akina mama
wajawazito kupatiwa huduma kwa ukaribu na maeneo wanayoishi na hivyo
kutekeleza lengo la Wizara ya afya na Ustawi wa jamii la kusogeza huduma
za afya umbali usiozidi kilomita nne kutoka kwenye makazi yao.
No comments:
Post a Comment