Waziri
Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm pamoja na Rais Jakaya Kikwete
wakiwasili katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya
Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya
LABIOFAM ya nchini Cuba.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amefurahishwa na uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua
viluwiluwi vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria kilichopo eneo la
viwanda, Tamco-Kibaha mkoani Pwani ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali
iliyojipangia ya kupambana na kupunguza vifo visababishwavyo na ugonjwa
huo.
Uzinduzi
huo ulifanywa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi zinazopambana na Malaria (ALMA).
Katika
uzinduzi huo, Rais Kikwete ameishukuru nchi ya Cuba kwani wao ndiyo
walikubali kutoa wataalamu pamoja na teknolojia ili kuisaidia Tanzania
kuendeleza sekta ya madawa ikiwemo kupambana dhidi ya ugonjwa wa malaria
pamoja na kuwafundisha wataalamu wa Tanzania ili waweze kuendeleza
kiwanda hicho.
Rais
Kikwete alieleza kwamba, akiwa nchini Cuba mnamo Novemba 2009
alitembelea viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali za kibaiolojia
kikiwemo kiwanda cha Biolarvicides cha LABIOFAM SA kinachomilikiwa na
Serikali ya Cuba hivyo Serikali hiyo ilipokubali awamu ya kwanza
ilipanga kujenga kiwanda cha Biolarvicides kwa lengo la kuua viluwiluwi
wa mbu wanaoeneza malaria ambapo mradi huo ndo umezinduliwa rasmi tarehe
2 Julai mwaka huu na pia katika awamu ya pili ilikuwa ni ujenzi wa
viwanda vya kuzalisha dawa mbalimbali kwa ajili ya kutibu na kuzuia
magonjwa ya binadamu na wanyama na mwisho ni awamu ya tatu ya ujenzi wa
viwanda vya dawa na vyakula vya ziada yaani Food supplement kwa ajili ya
watu wenye magonjwa ya kudumu na kuzalisha mbolea za kibaiolojia
(bio-fertilizers).
“Chimbuka
la ujenzi wa kiwanda hiki ni ziara yangu niliyoifanya nchini Cuba,
ndipo niliona kuna umuhimu wa kuiomba Serikali ya Cuba itusaidie
kutupatia teknolojia pamoja na wataalamu lakini pia niliagiza Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC) wajenge ushirikiano kwa ajili ya kutengeneza
kiwanda nchini Kwetu na matokeo yake ndo haya”, alisema Dkt. Kikwete
Rais
Kikwete alimshukuru Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Jorge Luis
Lopez kwa ushirikiano mkubwa aliouonyesha kwa kuisaidia Tanzania katika
kuhakikisha kwamba kiwanda hicho kinawepo nchini na kwa ukarimu wao
pasipo tamaa ya kutoa teknolojia hiyo, licha ya nchi yao kutakuwa tajiri
wao walitupati teknolojia hii na walishirikiana nasi katika ujenzi wa
kiwanda hicho pamoja na wataalamu
“Huu
ndiyo urafiki wa kweli na udugu nakuomba Balozi unifikishie salamu
zangu za dhati na shukurani zangu mimi pamoja na watanzania wote kwa
ajumla kwa Rais Raul Castro kwa mchango wake mkubwa kwa nchi yetu
Tanzania”, Alisema Dkt. kikwete.
Naye
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Jorge Luis Lopez ameziomba
nchini nyingine ziweze kuiga ushirikiano mkubwa wa Serikali ya Tanzania
na Cuba na pia kwa niaba ya Serikali yake amemshukuru Rais Kikwete kwa
utendaji kazi wake mzuri, uhusiano mzuri ambao ameujenga na kati ya
Tanzania na Cuba.
Naye
mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia na
Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi zinazopambana na Malaria (ALMA) na ametoa
pongezi zake za dhati na kueleza kwamba, hiyo ni hatua nzuri na kusema
kuwa kushuka kwa idadi ya vifo nchini Tanzania ni ishara ya uongozi
mzuri na bora wa Rais Kikwete na ishara nzuri kwa kuiacha nzuri katika
mahali pazuri pamoja mahali pazuri dhidi ya umaskini
Aidha,
ameeleza kuwa uwepo wa kiwanda hiko itakuwa ni ishara nzuri ya
mapambano na yeye kama Mwenyekiti wa Umoja wa nchi zinazopambana (ALMA)
dhidi ya malaria atazihamasisha nchi nyingine kutumia Afrika waweze
kutumia mazao yatokanayo na kiwanda hicho.
Kampuni
ya Tanzania Biotech Products Limited ni Kampuni iliyoundwa kwa ajili ya
kuendesha Kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua Viluwiluwi vya mbu
wanaoeneza malaria kilichopo Kibaha, Pwani ambacho kimejengwa kwa
kushirikiana na Kampuni ya LABIOFAM SA ya Cuba a kiwanda hiki kinatokana
na agizo l Rais Kikwete alilolito Januari 4 , 2010 kwa shirika la Taifa
la Maendeleo (NDC) baada ya ziara yake nchini Cuba.
Rais
Jakaya Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Desalegm wakiwa wamesimama kuimba nyimbo za taifa la Tanzania na
Ethiopia katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu
vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya
LABIOFAM ya nchini Cuba.
Baadhi
ya viongozi mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda
cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha.
Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa
ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.

Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm pamoja na mwenyeji wake Rais Jakaya
Kikwete wakizungumza jambo katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza
Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdala Kigoda akizungumza katika uzinduzi
wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Jiwe
la Msingi la Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa
Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza
Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki
kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza
Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki
kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na
Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Baadhi
ya wageni mbalimbali waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa
Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Waziri
Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm akizungumza katika uzinduzi wa
Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Balozi
wa Cuba nchini Tanzania Bw. Jorge Luis Lopez akiongea wakati wa hafla
ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya
mbu wanaoeneza malaria kilichojengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Cuba
na Tanzania, ambapo aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika
masuala balimbali ya maendeleo leo mkoani Pwani.
Waziri
Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm (wa nne kushoto) pamoja na Rais
Jakaya Kikwete (wa tano kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa
Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza
Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki
kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na
Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Waziri
Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm (kushoto) pamoja na Rais Jakaya
Kikwete (kulia) wakizinduwa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua
Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la
Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya
nchini Cuba.
Baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wakiwasili katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho.
Rais
Jakaya Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Desalegm wakiwa wamesimama kuimba nyimbo za taifa la Tanzania na
Ethiopia katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu
vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya
LABIOFAM ya nchini Cuba.
Waziri
Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm akizungumza katika uzinduzi wa
Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
No comments:
Post a Comment