utt

.

line

line

line of success

line of success

Thursday, July 2, 2015

UTT PID yatoa huduma za uuzwaji wa fomu za viwanja vyake kwa Wananchi wanaotembelea maonesho ya 39 ya Sabasaba


DSC_1257Afisa Masoko Bi.Kilave Atenaka   akitoa maelezo kwa mmoja wa  wananchi waliotembelea kwenye banda hilo lililopo jirani ya kuingia katika banda kubwa la Ukumbi wa Karume
Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID) ipo kwenye Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yanayoendelea katika mabanda ya Saba saba katika  viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa jijini.
Banda la UTT PID lipo  jirani na kuingia katika banda la Wizara ya fedha  upande wa kuingia kwenye banda la  ukumbi wa Karume. Hivyo wamewaomba wananchi  mbalimbali  wameombwa kujitokeza kupata huduma  mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwemo  huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo nchini ikiwemo vile vya mradi wa katika miji ya Chalinze na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akielezea Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka   katika maonyesho hayo, alibainisha kuwa mbali na uuzaji wa fomu kwa ajili ya viwanja, pia  wanatarajia kuanza kuuza kwa umma na taasisi mbalimmbali  miradi mipya  ikiwemo wa Tundwi songani-Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila Mkoani Morogoro.
Aidha, Bi Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbalimbali zitolewazo na  taasisi hapa nchini.
Kwa sasa UTT PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri katika utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
DSC_1218Moja ya mabango ya UTT PID  katika banda lao hilo ndani ya Saba saba..
DSC_1224
Mmoja wa  wananchi aliyetembelea katika banda la UTT PID, akisaini kitabu cha wageni wakati alipofika kujua shughuli mbalimbali za taasisi hiyo. anayeshuhudia kulia kwa mwananchi huyo ni Afisa Masoko  wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka
DSC_1199 baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa   Afisa Masoko  wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka   wakati walipotembelea katika banda hilo..
DSC_1250Afisa Masoko wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka  akiwa katika banda lao hilo tayari kwa kutoa huduma za taasisi hiyo kwa wananchi wanaotembelea ndani ya maonyesho hayo hayo ya 39 ya Sabasaba..
DSC_1219
DSC_1213Mmoja wa wanasheria wa UTT PID,  Bw. Lawrence Nzuki (kushoto) akitoa maelezo ya kitaalam kwa mwananchi aliyetembelea banda hilo la UTT PID,  kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa hapa nchini. aliyepo mbele ni Afisa Masoko wa UTT PID, Bi.Kilave Atenaka.

No comments:

Post a Comment