Wtaa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
BAADA ya hivi karibuni kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Viti
Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Morogoro Vijijini
alikozaliwa, staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ameibuka na kueleza
kwamba ameamua kufanya hivyo ili kuwatetea walemavu na watoto wa kike.
Akipiga stori na Ijumaa, Wastara alisema wananchi ambao ni walemavu
wamekuwa hawatendewi haki katika maeneo mbalimbali kulingana na maumbile
yao hivyo lengo lake kubwa ni kwenda kutetea haki zao ili ziwe sawa na
watu wengine pamoja na sanaa kwani wasanii wamekuwa wakinyonywa kutokana
na kazi zao kuuzwa hovyo. Naamini nitashinda, kwani jimbo nililochagua…
No comments:
Post a Comment