utt

.

line

line

line of success

line of success

Tuesday, June 30, 2015

Washindi wa tuzo za TANAPA 2014 wakabidhiwa tuzo Jjjini Mwanza

Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) , Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanahabari waliofanya vizuri katika uandishi wa masuala ya Uhifadhi.Hafla iliyofanyika katika Hotel ya Gorden Crest jijini Mwanza. 
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza katika hafla hiyo juu ya lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo kwa wanahabari nchini.
Mkuu wa wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Baraka Konisaga akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa Wanahabari waliofanya vizuri katika uandishi wa masuala ya Uhifadhi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza wakai wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa Tuzo zitolewazo na TANAPA kwa wanahabari.
Mkuu wa Majaji walioshiriki kupatikana kwa washindi wa tuzo zitolewazo na TANAPA kwa wanahabari, Dkt Ayoub Ryoba akizungumza katika hafla hiyo.
Dkt. Ryoba akitambulisha majaji wenzake walioshiriki katika kupata washindi.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akitoa ngao Vyeti pamoja na mfano wa Hundi kwa washindi wa tuzo za TANAPA 2014 zitolewazo kwa wanahabari
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Meja Jenerali Mrisho Sarakikya akizungumza katika hafla hiyo zaii akizungumzia historia ya namna alivyoshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 38.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo,Lazaro Nyalandu, akitunuku tuzo kwa Meja Jenerali, Mirisho Sarakikya pamoja na kitambulisho maalumu ambacho kitamuwezesha kuingia bila malipo katika hifadhi 16 za Taifa.
Meja Jenerali, Sarakikya akifurahia zawadi hiyo iliyotolewa na TANAPA.
Mwandishi wa Habari wa Channel ten Cassius Mdami akizungumza kwa niaba ya washindi wa tuzo hizo.
Mgeni rasmi, Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na washindi.
Mgeni rasmi ,Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na wahariri katika vyombo mbalimbali vya habari.
Mgeni rasmi, Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki katika hafla hiyo.(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko jijini Mwanza).
 
 

No comments:

Post a Comment