Profesa Sospeter Muhongo ni miongoni mwa makada wa CCM waliochukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwani kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. Katika makala haya mwandishi anazungumza na watu walio karibu na kada huyo wa CCM, ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini katika kashfa ya wizi kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, kabla hajasafishwa baadaye kwamba hahusiki.
Shemejji yake amsifu kwa uadilifu
Shemejji yake amsifu kwa uadilifu
“Wanaomtuhumu Profesa Muhongo kuhusu ufisadi
hawamfahamu. Huyu ni kati ya warithi sahihi wa Mwalimu Nyerere,
inapofikia suala la uadilifu na kutotumia cheo kujinufaisha,” anaanza
kueleza Bertha Mtaragara, shemeji mkubwa wa Profesa Muhongo.
Mtaragara anasema kwa tuhuma za ufisadi
zilipoibuka dhidi ya Profesa Muhongo, familia ilishtuka na kufadhaika
kupita kiasi kwa sababu inajua tabia yake kuwa siyo fisadi, mla rushwa
wala mpenda maslahi binafsi.
“Binafsi nilimpigia simu na kumuuliza ukweli wa
jambo hilo iwapo kweli amehusika. Aliponisisitizia na kunithibitishia
hajausika nikamsisitiza amwachie Mungu kwani ndiye mwamuzi wa haki. Na
hakika ukweli umedhihiri baada ya uchunguzi kuwa hakuhusika,” anasema
Mama Mtaragara na kuongeza:
“Tunaomfahamu Muhongo tangu utoto hatuamini kama
kweli anaweza kubadilika kiasi cha kufikia hatua ya kuibia jamii yake
ili ajinufaishe binafsi kwa sababu siyo tabia yake,”
Anasema familia ililazimika kufunga na kuomba
kashfa ya Escrow ilipoibuka ili ukweli ubainike iwapo Profesa Muhongo
alihusika au la.
“Baada ya suala la Escrow kumalizika, familia
nzima akiwemo Profesa Muhongo na mkewe Bertha, tulienda nyumbani kwa
kaka mkubwa wa familia Kingi Musiba kufanya ibada ya kumshukuru Mungu,”
anabainisha Mama Mtaragara.
Tabia ya Muhongo tangu utoto
“Kusema ukweli bila kujali mhusika wala madhara
yanayoweza kumkuta kwa kuusema ukweli huo ni moja kati ya sifa na tabia
ya Profesa Muhongo tangu utoto,” anasema Mama Mtaragara
“Hakuwahi na ninaamini hatakuwa na tabia ya
kufurahisha watu kwa maneno ya sifa bandia. Wakati mwingine tabia hii
ilimfanya kukosa marafiki kutokana na watu wengi kupenda kupambwa kwa
maneno ya uongo,” anabainisha na kuongeza;
No comments:
Post a Comment