Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu
Tanzania, Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa
nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na
stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na
waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za
kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za
TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za
kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.
![](//3.bp.blogspot.com/-3_JpsrkQKS0/VYkqz17rjfI/AAAAAAAAhAA/D5s_StXfzw0/s640/DSC_1312.JPG)
Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu
Tanzania, Bw. Moses Mwanyilu akionyesha filamu kutoka nje ambayo
inasemekana kuwa na maadili yasiofahaa kutazamwa na watoto chini ya
miaka 18 ambayo inaendelea kuuzwa nchini huku ikiwa haijakaguliwa na
bodi ya filamu wala haina stika za TRa kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza
watayarishaji na wauzaji wa filamu za kitanzania ambazo zimekuwa na
mlolongo mrefu hadi kuingia sokoni.
![](//2.bp.blogspot.com/-1LgphyauTkM/VYkrDgMpM3I/AAAAAAAAhAQ/K71DSavJc5E/s640/DSC_1322.JPG)
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa.
![](//4.bp.blogspot.com/-amlvxh_Bwv4/VYkrJhZPpoI/AAAAAAAAhAY/Eqkr-_UG6CY/s640/IMG_0608.JPG)
Mjumbe wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah
akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia
tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za
filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu
kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka
husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili.
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na
waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao
bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu
kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za
nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu
kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita
kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku
wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya
filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani
zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.
Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa
Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya
Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao
na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi
kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea
kupeleka filamu sokoni.
No comments:
Post a Comment