utt

.

line

line

line of success

line of success

Wednesday, July 15, 2015

LOWASSA ATOA TAMKO,KINGUNGE: MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM ULIKUWA BATILI SOMA HAPA>>>>


LEO Mzee Kingunge kaongea na vyombo vya habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.
Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika kuwajadili wagombea"
Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba kukata majina ya wagombe.
Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama.
Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.
Kwa mujibu wa Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.

Kingunge amewapongeza sana kina Kimbisa, Nchimbi na Sophia kukataa maamuzi ya Kamati Kuu, waliisamamia Katiba ya Chama.

Kingunge anadai CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani.

Kingunge anasisitiza, Kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote.

Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.

Kingunge anadai Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili kupata ushindi - chama kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu Lowassa na kuongeza kuwa anaamini Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata sapoti hiyo.

Anadai Kabla ya Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili wakubaliane na kukosoana lakini mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja ili kupambana na adui.
Mwisho amemalizia kwa kusisitiza: “Yaliyotokea Dodoma si halali na si haki…”
Asanteni

(CREDIT: JAMII FORUMS)

No comments:

Post a Comment