![](http://2.bp.blogspot.com/-Wfm8dO1_50Q/VZo8XgpAZ-I/AAAAAAAAe3Q/QPZnlFKfAHM/s640/p11.jpg)
Meya
wa Ilala, Jerry Slaa akifuatilia kwa karibu burudani zilizokuwa
zinatolewa na vikundi mbalimbali katika mkutano huo. Pamoja nae ni
Mbunge wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa NEC wa CCM,Alhaji Adam Kimbisa.
![](http://1.bp.blogspot.com/-MiegnJV85NU/VZo8YxKfvHI/AAAAAAAAe3Y/1ald8MaJYj4/s640/s1.jpg)
Diwani
wa kata ya Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Slaa
akihutubia wananchi katika uwanja wa shule ya msingi kitunda mwishoni
mwa wiki ambapo alieleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi
chake cha uongozi na kukamilisha ahadi mbalimbali alizokuwa amezitoa.
![](http://4.bp.blogspot.com/-XaXT_YVhKBA/VZo8bd64gxI/AAAAAAAAe3o/_IajlyM0g2k/s640/p3.jpg)
Mmoja
wa wawakilishi wa kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya
wenzake kutoka kwa Meya wa Manispaa ya ilala ambazo alikuwa amewaahidi
wakati wa mkutano wa Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
![](http://2.bp.blogspot.com/-f1t-VxO9c6k/VZo8bKTP3eI/AAAAAAAAe3w/rpvwHXbuERo/s640/p5.jpg)
Baadhi
ya madiwani na wazee wa Ukonga wakimpongeza Meya Jerry Slaa kwa
kutimiza ahadi alizotoa muda mfupi baada ya kueleza mafanikio
yaliyopatikana chini ya uongozi wake ambapo vilevile alitangaza nia ya
kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga.
![](http://1.bp.blogspot.com/-obOW2xt7N04/VZo8b3rJoBI/AAAAAAAAe3s/492PrRxYNZM/s640/p6.jpg)
Watoto wakitoa burudani wakati wa mkutano huo.
![](http://2.bp.blogspot.com/-F5zFSFDXIog/VZo8dJM3rMI/AAAAAAAAe38/u4DFYE4lztY/s640/p7.jpg)
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wakishangilia kwa furaha baada ya kuguswa na hotuba ya Meya Jerry Slaa.
![](http://4.bp.blogspot.com/-fTyKO5jkYRw/VZo8ahblcXI/AAAAAAAAe3g/jbHbuQ0eqQE/s640/p10.jpg)
Baadhi ya madiwani na viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment