Mbunge Mgimwa akitimiza ahadi yake ya bati 50 kwa kituo cha yatima Tosamaganga |
Mbunge Mgimwa katikati akitazama nguzo za umeme katika kata ya Mgama.
WAKATI wabunge wakiwa mbioni
kumaliza muda wao mbunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa amesema
kuwa kwa kipindi chake cha mwaka mmoja kama mbunge wa jimbo hilo la
Kalenga amesema anamshukuru Mungu katika safari yake ya kuwatumikia
wananchi wa jimbo la Kalenga kwa kufanikisha kutekeleza ahadi zake
kwa asilimia 99.9 ndani ya mwaka mmoja .
Huku akiwaomba wananchi wa jimbo hilo la Kalenga kuweza kumpima kwa kazi alizozifanya kwa mwaka mmmoja na zile zilizofanywa na wabunge waliotangulia katika jimbo hilo na wabunge wa upinzani kwa kipindi cha miaka mitano walioongoza majimbo yao. Bw. Mgimwa aliyasema haya jana wakati akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM na ahadi mbali mbali zilizoahidi mbunge aliyetangulia Marehemu Dk. Wiliam Mgimwa kwa kila kata kati ya kata 13 za jimbo la Kalenga . Alisema kuwa katika kata ya Kiwere ahadi ambazo amezitekeleza ni pamoja na mradi wa umeme vijiji vya Mgera ,kitapilimwa,Mfyome ambao unaendelea pia Mradi wa Maji, Mfyome na kiwere unaendelea, Bati 80 shule ya msingi Kiwere,Bati 50 Itagutwa,vikundi vya vicoba kata ya kirewe vimepewa Tsh milioni 3,ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kiwere amechangia milioni 2 ujenzi wa bweni sekondari ya Kiwere amechangia Tsh milioni 1kata ya Nzihi katika shule ya Dintyus sekondari amechangia Tsh milioni 2, saruji mifuko 100,Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kidamali na mifuko 50 ya saruji, Tsh 400,000 kwa timu ya daraja la tatu ngazi ya Mkoa wakati kata ya Ulanda Shule ya msingi Lukwambe Bati 100, ujenzi wao kituo cha afya Mlangali mchango wa Tsh 250,000,mradi wa maji kijiji cha Mwambao,kijiji cha Weru ,mradi wa umeme Kijiji cha Ibangamoyo, Kibebe na Weru Mchango wa Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara Shule ya sekondari Kalenga.
Mbunge Mgimwa alisema kwa kata
ya Kalenga kwa shule ya msingi amechangia Tsh 660,000 kwa ajili ya
ujenzi wa vyoo vya wanafunzi,Bati 50 na mabelu ya nguo za yatima
Tosamaganga vyote vikiwa na thamani ya Tsh milioni 3.5 pia amechangia
Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara Sekondari ya Lipuli ,mifuko 50 ya
Saruji,Vicoba kijiji cha kalenga Tsh 500,000 pamoja na vifaa vya michezo
kwa vijana
Huku kata ya Mseke katika shule ya msingi Ugwachanya Bati 60 , shule ya msingi Sadani Bati 60 na saruji 50 na Tsh milioni 1, shule ya msingi Makota Bati 50 Mseke sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara,kikundi cha Sliki Tanangozi Tsh 700,000. Mradi wa umeme kijiji cha Wenda unaendelea wakati kata ya Luhota kwa upande wa Shule ya msingi Wangama Bati 50 na saruji 50, kikundi cha siliki Tagamenda Tsh 500,000 na Luhota sekondari Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa maabara Alitaja kata nyingine ambazo amechangia kuwa ni Magulilwa kwa shule ya msingi Nega B Bati 100,kijiji cha Mranda Bati 80, mradi wa umeme Nega B na Magulilwa unaendelea, shule ya msingi Ng’enza Saruji mifuko 50 ,Visiwa viwili vya maji na shule ya sekondari Muwana Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara na kata ya Lyamgungwe Kijiji cha Malagosi Bati 80 za ujenzi wa zahanati,kijiji cha Lupembelyasenga saruji 50 , mradi wa umeme Wenda,Kikombwe,Ismila na maji kijiji cha Kikombwe unaendelea Kuchangia Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Ismila Pia kata ya Mgama kwenye shule ya msingi Mgama Bati 100 na Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, shule ya msingi Ibumila Bati 50 na saruji 50 ,shule ya msingi Itwaga saruji 20, shule ya msingi Luhato madawati 30 na mradi wa umeme kijiji cha Mgama unaendelea na kata ya Ifunda amechangia Shule ya msingi Mibikimitali Bati 50, Shule ya msingi Udumuka saruji 100,kijiji cha Mfukulembe Bati 50 ,shule ya sekondari Lyandembela milioni 2 ujenzi wa maabara na Shule ya sekondari Lyasa Tsh milioni 2. Bw. Mgimwa alisema kuwa kwa kata Lumuli, kijiji cha Isupilo Bati Bati 50, kijiji cha Muwimbi Bati 80 ,Lumuli sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa Maabara,mradi wa umeme Isupilo, Itengulinyi, mradi wa maji Isupilo ,Itengulinyi na Lumuli inaendelea pia kivuko cha barabara ya Itengulinyi – Magunga kimekamilika wakati kata ya Wasa ,Shule ya msingi Usengelendeti Bati 100,Mahanzi Bati 80,WASA sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara, mradi wa umeme unaendelea Alitaja utekelezaji wa ahadi alioufanya pia kata ya Maboga katika Shule ya msingi chamgogo Bati 50 , Shule ya msingi Kidilo bati 50, Shule ya sekondari Kiponzero Milioni 2 ujenzi wa maabara , barabara ya Magunga – Makota umekamilika,shule ya msingi Makombe saruji mifuko 50 pia mradi wa umeme Kiponzero unaendelea. Mbunge huyo alisema kuwa jimbo la Kalenga kuna jumla ya kata 13 ila sasa ni kata 15 ambazo zimetokana na kata mpya na kuwa kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 110 amepata kuzitumia kutimiza ahadi zake kwa kipindi chake cha mwaka mmoja pekee aliopata kuwepo madakarani. Hata hivyo alitaja ahadi ambazo bado kuzitimiza na atazitimiza wakati wowote kabla ya kumaliza muda wake kuwa ni ahadi ya Tsh milioni 1 kwa ajili ya Vicoba Ifunda kibaoni ,bati 100 kwa ajili ya kuchangia ujenzi shule ya wasichana Ifunda ,ahadi ya Tsh milioni 1 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki katika Kanisa la Lutherani Ifunda kibaoni na ahadi ya mwisho ni ya bati 60 kwa ajili ya shule ya sekondari Lyandembela Hivyo aliwataka wananchi wa jimbo la Kalenga kuendelea kuwa na imani zaidi kwani amefanikiwa kutimiza ahadi zilizonyingi ambazo amepata kuzitoa kwa muda wa mwaka mmoja pekee na kuwa iwapo watamchangua tena basi wawe na imani ya kupata maendeleo makubwa zaidi ya haya . “Naomba wananchi wa Kalenga niwahakikishie kuwa nitagombea tena Ubunge kwa mwaka huu ili niweze kupata miaka yangu mitano ya kushirikiana nanyi katika kuleta maendeleo “ |
No comments:
Post a Comment