utt

.

line

line

line of success

line of success

Tuesday, June 30, 2015

MBUNGE MBATIA AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA KIJIJINI KWAO KWAMARE JIMBONI VUNJO.

Mbunge wa kuteuliwa,Mh James Mbatia akiwasili katika kijiji cha Kirua Vunjo Magharibi na kupokelewa na msaidizi wake Hamis Hamis kwa ajili ya zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia BVR.
Mbunge wa kuteuliwa ,Mh James Mbatia akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasil katika kijiji cha Kwamare kata ya Kirua Vunjo Magharibi Jimbo la Vunjo kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Mbunge James Mbatia akitoa maelezo yake kwa mmoja wa maofisa wa zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kupita mfumo wa BVR.
Mbunge James Mbatia akichukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la uandikishaji katika kijiji cha Kwamare kata ya Kirua Vunjo.
Mh Mbatia akitia saini katika kifaa kimoja wapo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu.
Mh Mbatia akiweka vidole gumba kwa ajili ya kuchukuliwa alama.
Afisa uandikisha akimkabidhi Mh Mbatia kitamburisho chake mara baada ya kumaliza zoezi la uandikishaji.
Mh Mbatia akionesha kitamburisho maalumu kwa ajili ya zoezi la kupiga kura litakalofanyika hapo baadae mwezi oktoba.
Msaidizi wa Mh Mbatia ,Hamis Hamis akikabidhiwa kitamburisho chake mara baada ya kumaliza zoezi la

NSSF yatoa huduma za afya bure Maonesho ya Sabasaba

Mmoja wa Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mbele aliyekaa akitoa huduma katika Banda lao kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba. viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiwahudumia wateja wao.
Mmoja wa Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mbele aliyekaa akitoa huduma katika Banda lao kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba. viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam wakiwahudumia wateja wao.
IMG_01411-988x1024
Dk. Suzan Lymo toka Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam (wa kwanza kulia) akimuhudumia mteja akipatiwa huduma za afya bure zinazotolewa na NSSF.
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakitoa huduma katika Banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba. viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tayari kwa kuwahudumia wateja wao.
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakitoa huduma katika Banda la NSSF kwenye maonesho 39 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba. viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tayari kwa kuwahudumia wateja wao.

Edwin Ngonyani Mkurugenzi Mtendaji mpya wa STAMICO

Mkurugenzi2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mhandisi Edwin Amandus Ngonyani kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico). Uteuzi huo umeanza Jumapili iliyopita, Juni 28, 2015.
Taarifa ya kuthibitisha uteuzi huo iliyotolewa Ikulu, Dar es salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) leo, Jumanne, Juni 30, 2015, inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Mhandisi Ngonyani alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Migodi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico.
Mhandisi Edwin Ngonyani ni mhandisi wa migodini mwenye uzoefu wa muda mrefu wa sekta ya madini. Anayo shahada ya kwanza ya fani hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Zambia na shahada ya uzamili (MSC) kwenye fani hiyo hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Exeter, Camborne School, Uingereza.
Mhandisi Ngonyani amefanya kazi nzuri wakati anakaimu nafasi ya Ukurugenzi Mtendaji na kwa kumteua, Rais Kikwete ana imani kubwa kuwa ataendeleza kazi hiyo nzuri ya kuimarisha uwekezaji wa umma katika sekta hiyo ya madini kupitia Stamico.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
30 Juni, 2015

Wasambazaji wa filamu kugoma kulipa kodi ifikapo 1/7/2015

Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.
Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw. Moses Mwanyilu akionyesha filamu kutoka nje ambayo inasemekana kuwa na maadili yasiofahaa kutazamwa na watoto chini ya miaka 18 ambayo inaendelea kuuzwa nchini huku ikiwa haijakaguliwa na bodi ya filamu wala haina stika za TRa kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza watayarishaji na wauzaji wa filamu za kitanzania ambazo zimekuwa na mlolongo mrefu hadi kuingia sokoni.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa.
Mjumbe wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili.
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.
Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.

Wauza mafuta wapewa onyo

SERIKALI imesema itawachukulia hatua kali wafanyabiashara wa mafuta, ikiwamo kuwafungia vituo vyao na pia kufuta leseni zao watakaobainika kugoma kuuza nishati hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage amewaonya wamiliki wa vituo vya mafuta nchini wasije wakajiingiza katika mtego wa kufanya mgomo wa kuuza mafuta katika vituo vyao.
Mwijage alitoa tamko hilo wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo Naibu Spika, Job Ndugai alimtaka atoe tamko la Serikali kutokana na taarifa zilizokuwa zikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba wauza mafuta wamepanga kugoma kuuza mafuta kuanzia leo ili kusubiri bei mpya ya bidhaa hiyo. Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage

Rais Mugabe aomba kufunga ndoa na Obama.

Obama Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amempa changamoto Rais wa Marekani, Barrack Obama, baada ya kumwomba  mkono wake kwenye ndoa. Maoni ya Rais Mugabe yanakuja baada ya ndoa za mashoga kuhalalishwa Marekani na mahakama kuu. Kwenye mahojiano ya
kila wiki na redio ya Zimbabwe, Jumamosi iliyopita Rais Mugabe alisema amehitimisha kuwa Obama anaunga mkono ndoa za jinsia moja, kuwatetea mashoga na hata kufurahia machoni pake kuyaona hayo. Alisema hivi karibuni atafunga safari na kwenda Washington DC ampigie goti na kumwomba waoane.
Katika hatua nyingine, Mugabe alisema serikali ya Marekani inapotoshwa na kuendeshwa na waabudu shetani wanaotusi Taifa la Marekani. Aliongeza kuwa mila hiyo ya Marekani na urithi, ulikuwa unalenga kanuni za mkristo, lakini ni hasara kubwa kwa Taifa zima la Marekani kwa dhana ya kishetani ya wanasiasa walarushwa nchini humo.
Muhuri wa Obama kuhusu ndoa za mashoga, umekuwa wa kwanza kutokea tangu rais kukaa madarakani. Kulikuwa na ongezeka la shinikizo kwa ajili ya rais kufafanua maoni yake ya awali ya mchanganyiko huo. Wanachama wawili waandamizi wa utawala wake walitangaza msaada binafsi kwa ajili ya ndoa mashoga na siku moja baadaye wapiga kura katika Jimbo la Carolina walipitisha hali hiyo ambayo inaleta mabadiliko ya katiba iliyofafanua ndoa kama muungano kati ya mwanaume na mwanamke.

Washindi wa tuzo za TANAPA 2014 wakabidhiwa tuzo Jjjini Mwanza

Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) , Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanahabari waliofanya vizuri katika uandishi wa masuala ya Uhifadhi.Hafla iliyofanyika katika Hotel ya Gorden Crest jijini Mwanza. 
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza katika hafla hiyo juu ya lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo kwa wanahabari nchini.
Mkuu wa wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Baraka Konisaga akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa Wanahabari waliofanya vizuri katika uandishi wa masuala ya Uhifadhi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza wakai wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa Tuzo zitolewazo na TANAPA kwa wanahabari.
Mkuu wa Majaji walioshiriki kupatikana kwa washindi wa tuzo zitolewazo na TANAPA kwa wanahabari, Dkt Ayoub Ryoba akizungumza katika hafla hiyo.
Dkt. Ryoba akitambulisha majaji wenzake walioshiriki katika kupata washindi.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akitoa ngao Vyeti pamoja na mfano wa Hundi kwa washindi wa tuzo za TANAPA 2014 zitolewazo kwa wanahabari
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Meja Jenerali Mrisho Sarakikya akizungumza katika hafla hiyo zaii akizungumzia historia ya namna alivyoshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 38.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo,Lazaro Nyalandu, akitunuku tuzo kwa Meja Jenerali, Mirisho Sarakikya pamoja na kitambulisho maalumu ambacho kitamuwezesha kuingia bila malipo katika hifadhi 16 za Taifa.
Meja Jenerali, Sarakikya akifurahia zawadi hiyo iliyotolewa na TANAPA.
Mwandishi wa Habari wa Channel ten Cassius Mdami akizungumza kwa niaba ya washindi wa tuzo hizo.
Mgeni rasmi, Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na washindi.
Mgeni rasmi ,Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na wahariri katika vyombo mbalimbali vya habari.
Mgeni rasmi, Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki katika hafla hiyo.(Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko jijini Mwanza).
 
 

MO ASSURANCE yajipanga kutoa huduma bora kwa watanzania maonyesho ya Sabasaba

IMG_5136
Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE),  Ravinshankar Venkatrama ( wa pili kushoto) akiwa na timu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo watakaokua wanatoa huduma katika Banda la MO ASSURANCE lilipo ndani ya mabanda ya MeTL Group kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere,  barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa wa kampuni ya MO ASSURANCE, Mariot Ndomba, Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack pamoja na  Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya MO ASSURANCE, Esther Moringi.
MO Assurance kampuni ya bima inayohudumia nchi nzima kwa kutoa huduma mbalimbali za bima za majanga ikiwemo ajali ya moto, bima ya wizi, bima za ajali mbalimbali.
“MO Assurance tunapatikana ndani ya jengo la CRDB  gorofa ya nane, mtaa wa Azikiwe ambapo tunatoa huduma mbalimbali za bima.” alibainisha meneja masoko msaidizi, Esther Moringi.
Aidha, kwa sasa MO Assurance yenye kauli mbiu ya ‘Amani zaidi, Uhakika zaidi’ ina matawi sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Singida, Arusha na kwingineko.  Pia kwa sasa ni miongoni mwa makampuni ya  bima nchini yaliyofanikiwa ikiwemo kutoa huduma kwa wateja wa aina tofauti wakiwemo wa ndani na nje wanaoishi nchini.
Kampuni ya MO Assurance ni kampuni Mama ya MeTL Group ambapo unaweza kuwasiliana nao kupitia barua pepe: infomoa@moassurance.co.tz ama kutembelea mtandao wao kupitia : moassurance.co.tz 
IMG_5122
Kutoka kushoto ni Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE),  Ravinshankar Venkatrama, Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya mo ASSURANCE, Esther Moringi, Afisa wa MO ASSURANCE, Mariot Ndomba pamoja na Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack katika picha ya pamoja wakiwa tayari kutoa huduma kwa wateja mbalimbali watakaotembelea katika Banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere,  barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
IMG_5118
Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack akipiga ‘selfie’ na wafanyakazi wenzake.
IMG_5210
 Ofisa Mtendaji wa Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack katika picha ya pamoja na mbunifu wa mavazi nchini, Ally Rehmtulah alipotembelea banda la MO ASSURANCE.
IMG_5234
Muonekano wa nje wa banda la kampuni ya MO ASSURANCE ndani ya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa yalioanza kurindima katika viwanja vya Sabasaba katika barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.